Zifuatazo ni hatua zinazoonesha mlolongo wa uchapishaji wa makala katika JADAKI:
(I) Mhariri Mkuu au Mhariri Msaidizi atatoa wito wa toleo la makala.
(II) Mwandishi atawasilisha kwa njia ya mtandao (kupitia submission portal) muswada wa makala yake ambao umezingatia maelekezo yote yaliyotolewa katika sehemu ya maelekezo kwa waandishi.
(III) Mhariri Mkuu pamoja na Mhariri Msaidizi watafanya uhakiki wa awali wa miswada ya makala iliyotumwa ili kuona kama waandishi wamefuata maelekezo husika.
(IV) Miswada yote ambayo haijafuata taratibu za awali itakataliwa kabla ya kupelekwa kwa wasomaji/wahakiki.
(V) Kupeleka miswada ya makala kwa wataalamu wa nyuga ambazo waandishi wamemakinika nazo. Kabla makala hazijatumwa kwa wasomaji (wataalamu), yataondolewa majina ya waandishi ili kuzingatia itikeli za mchakato wa uchapishaji. Kila muswada utapelekwa kwa watalamu wasiopungua 2. Wataalamu hao wakimaliza kupitia miswada, watatuma mrejesho kwa Mhariri Mkuu au Mhariri Msaidizi. Aidha, watajaza fomu maalumu na watatoa maoni yao kuhusu kufaa au kutofaa kwa makala hiyo.
(VI) Mwandishi atatumiwa mrejesho wa muswada wa makala yake kutoka kwa Mhariri Mkuu au Mhariri Msaidizi baada ya kusomwa na wataalamu husika. Kulingana na uzito wa maoni yaliyotolewa, Mhariri Mkuu au Mhariri Msaidizi atapima na kutoa maamuzi mojawapo kati ya haya:
-
- Marekebisho Makubwa; haya yanahusisha mwandishi kupewa muda mwingi kuweka vema makala yake. Hivyo, atashauriwa aitume katika wito wa toleo lijalo baada ya kufanyia kazi maoni/marekebisho makubwa.
- Marebisho madogo; mwandishi atapewa muda mfupi, usiozidi wiki 2 kwa ajili ya kufanyia kazi maoni yaliyotolewa.
- Muswaada kukataliwa; huu ni mrejesho kwa mwandishi ambaye andiko lake halina hadhi ya kuwa makala ya kitaaluma.
Aidha, kutegemeana na jinsi mwandishi anavyotekeleza maoni yaliyotolewa, wakati mwingine anaweza kulazimika kupokea maoni mara nyingi kwa maana ya kuboresha andiko lake. Hii itatokea pale ambapo mwandishi hajatekeleza kikamilifu maoni yaliyotolewa; hivyo, matokeo yake, yatarudishwa tena maoni ili azidi kuyafanyia kazi hadi pale makala hiyo itakapokuwa sawa.
(VII) Kuandaa toleo la makala
Baada ya waandishi kukamilisha / kufanyia kazi maoni yaliyotolewa na wataalamu na Mhariri Mkuu na/au Mhariri Msaidizi, miswada ya makala itakusanywa na kuandaa toleo. Muswada wa toleo utatumwa kwa Wajumbe wa Bodi ya Uhariri ili waweze kupitia na kushauri kama toleo hilo linakidhi viwango vya kuchapsihwa. Baada ya hapo, maoni ya Bodi ya Uhariri yatafanyiwa kazi, kisha toleo la makala litachapsihwa.