Maelekezo kwa Waandishi

Yafuatayo ni masuala yatakayotakiwa kuzingatiwa na waandishi katika uandishi wa makala za  JADAKI:

I. Lugha ya uandishi wa makala ni.

II. Makala itatakiwa kuonesha maarifa mpya bayana; makala itatarajiwa kuwasilishwa katika mtiririko wenye mantiki na rahisi kwa msomaji kuelewa/kupata ujumbe.

III. Lugha rasmi na kitaaluma itatakiwa kuzingatiwa; mwandishi aepuke lugha isiyo rasmi na lugha ya kimazungumzo. Kabla mwandishi hajatuma makala yake, aipitie kwanza vizuri na kujiridhisha kuwa makosa yote yamerekebishwa kwa kiwango kinachoridhisha.

IV. Makala ipigwe chapa kwa kutumia programu ya Word kwenye hati ya Times New Roman yenye ukubwa wa 12. Nafasi inayotakiwa kati ya mstari na mstari ni 1.5.

V. Ukurasa wa kwanza uwe na taarifa hizi: anwani (mada), jina la mwandishi/waandishi, nambari ya simu, anuani ya baruapepe na taasisi au asasi (kama ipo). Taarifa hizo zifuatiwe na ikisiri inayoeleweka na inayotoa vema ufupisho stahiki wa makala, isizidi maneno 250 lakini isipungue maneno 100.

VI. Makala iwe na maneno kati ya 3000 hadi 7500.

VII. Marejeleo yafuate mfumo wa APA, Toleo la Sita kama inavyoonekana katika mifano ifuatayo:

Kitabu

Walker, J. (2006). Fitness and the urban walker. London: Blandford.

Sura katika Kitabu

Sera ya Lugha nchini Tanzania. Katika. Daud M. ( Mh.) Kiswahili na Maendeleo. Dar es Salaam: TUKI

Makala kutoka katika Jarida

Harsh, C., & Martin, G. (2013). Nafasi ya makongamano ya Kiswahili katika  kukuza Kiswahili:

Jarida la CHALUFAKITA. 1, 15-30

Tasnifu

Kazinyingi, M. (2020) Namna ya Kukabiliana na Korona Ulimwenguni: Mfano kutoka Tanzania. Tasnifu ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kiungo kifuatacho kina taarifa zaidi kuhusu urejeleaji kwa kuzingatia APA Toleo la Sita:

https://www.google.com/url?q=https%3A%2F%2Fwww.dcu.ie%2Fsites%2Fdefault%2Ffiles%
2Flibrary%2Fapaguide2016.pdf&sa=D&sntz=1&usg=AFQjCNFrJIm0AZv2zXsVhWx92DV-bpNxFQ">